Samedi 11 mai 2024

Archives

FORSC yatoa wito kwa rais ili muswada wa sheria ya Tume ya Ukweli na Maridhiano urekebishwe

05/05/2013 Commentaires fermés sur FORSC yatoa wito kwa rais ili muswada wa sheria ya Tume ya Ukweli na Maridhiano urekebishwe

Muungano huo wa mashirika ya kiraia, FORSC unabaini kua umekwishamtumia rais wa Jamhuri mapendekezo ya mabadiliko yanatakiwa kwenye muswada huo kabla ya kupasishwa bungeni. Kando ya hayo muungano huo umemtumia pia rais wa Jamhuri muswada wa sheria ya Mahakama Maalum kwa ajili ya Burundi.

<doc2444|left>Mapendekezo hayo ya Muungano huo wa mashirika ya kiraia yanatolewa baada ya wito wa Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty international kwa wanasiasa wa Burundi ambao wanatakiwa kuufanyia mabadiliko muswada huo wa sheria ya Tume ya Ukweli na Maridhiano ili kuheshimishwe haki za raia waliathirika kutokana na machafuko yaliyoikumba Burundi, kufuatia ukiukwaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Kunatakiwa kuwepo hakimu maalum kwenye Tume hio.

Kwa mujibu wa Bw. Pacifique Ninihahazwe, kiongozi wa muungano wa mashirika ya kiraia, FORSC, katika mapendkezo yenyewe inatakiwa Tume hio ya Ukweli na Maridhiano ipewe kisheria majukumu ya kuweza kufanya uchunguzi, msako na kuwaitisha washakiwa. Na hapa kuna ulazima uhusiano au ushirikiano baina Tume hio na Mahakama Maalum kwa ajili ya Burundi uwekwe wazi.

Muungano huo wa mashirika ya kiraia, FORSC unaomba upande wa makamishna watakaoongoza Tume hio kuwepo raia wa Burundi na raia kutoka ugenini ili taasisi hio iaminiwe na iwe na uwezo kisheria ya kuamuwa kuhusu makosa ya jinai yasiyosamehewa kama mauaji ya kimbali au uhalifu wa kivita.

Muungano huo wa mashirika ya kiraia unaomba pia katika mapendekezo yake kuhusu muswada wa sheria ya Tume ya Ukweli na Maridhiano, makamishna watakaoongoza Tume hio, 3 wateuliwe kutoka ugenini 2 kutoka mashirika ya kiraia, 2 wawe ni wanadini, 2 watoke upande wa vyuo au wawe ni wanasheria na hatimae 2 wapendekezwe na serekali. Muungano huo wa mashirika ya kiraia unaomba baraza la washauri kutoka ugenini kwenye Tume hio lifutiliwe mbali.

Kiongozi wa muungano wa mashirika ya kiraia, FORSC, Bw. Pacifique Ninihahazwe, anakiri kua na imani kwamba mapendekezo hayo yatatiliwa maanane. Anahakikisha kua katika mpango huo wa kuunda taasisi za Sheria ya mpito kuna mapendekezo ambayo yaliishatekelezwa na serekali.

Mfarakano

<doc2443|right>Wakati muungano huo wa mashirika ya kiraia ukiomba mapendekezo hayo yapewe umuhima na wakati shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International likiwaomba wanasiasa wa Burundi wafanye kila waliwezalo ili muswada wa sheria ya Tume ya Ukweli na Maridhiano ufanyiwe mabadiliko, wanasiasa wenyewe wanaonekana kutoelewana kuhusu uundwaji wa taasisi hio wakati huu, katika mazingira ya mvutano wa kisiasa.

Kwa mujibu wa bwa Frédéric Bamvuginyumvira naibu kiongozi wa chama cha Sahwanya-Frodebu cha upinzani, kabla ya yote kuna ulazima kuanzishwe mazungumwo baina upinzani na serekali ya Burundi ili kuwepo hali shwari na nyoyo zitulie, la sihivo kuna hatari kuwepo Tume ya kwanza na ya Ukweli na Maridhiano na Tume ya pili ya Ukweli na Maridhiano.

Upande wake katibu mkuu wa chama tawala cha CNDD FDD, Gélase Daniel Ndabirabe anasema huu ndiwo wakati mzuri wa kuunda Tume hio ya Ukweli na Maridhiano licha ya musukosuko ya kiuchumi au ya kiusalama. Matatizo hayo hayawezi kamwe kuathiri mpango huo, anasema katibu mkuu huyo wa chama tawala cha CNDD FDD. Ima kuhusu pesa za matumizi, mwanasiasa huyo anakiri kuwa zitapatikana sababu kuna wafadhili ambao wana nia ya kuiunga mkono serekali katika mpango huo wa kurejesha mwafaka nchini Burundi.

Hali ya usalama unaojiri nchini Burundi wakati huu ni pingamizi kubwa dhidi ya mafanikio ya mpango huo, anasema hayo bii Jeannine Nahigombeye kutoka muungano wa mashirika ya kiraia yanayofuatilia kwa karibu uundwaji wa taasisi zaihusuzo sheria ya mpito.

Kwa mujibu wa kiongozi wa Halmashahuri Huru ya Haki za Binadamu nchini Burundi, Emmanuel Ntakarutimana suala la kuiunda au la Tume ya Ukweli na Maridhiano wakati huu bado ni kitendawili. Tangu zamani inasemekana kuna ulazima tume yenyewe ibuniwe walakin ilionekana mazingira si ya kuridhisha na suali ni kujua ni lini hali itaonekana ni shwari. Kilicho dhahiri ni kwamba mpango unaendelea, anasema kiongozi wa Halmashahuri Huru ya Haki za Binadamu.

A nos chers lecteurs

Nous sommes heureux que vous soyez si nombreux à nous suivre sur le web. Nous avons fait le choix de mettre en accès gratuit une grande partie de nos contenus, mais une information rigoureuse, vérifiée et de qualité n'est pas gratuite. Nous avons besoin de votre soutien pour continuer à vous proposer un journalisme ouvert, pluraliste et indépendant.

Chaque contribution, grande ou petite, permet de nous assurer notre avenir à long terme.

Soutenez Iwacu à partir de seulement 1 euro ou 1 dollar, cela ne prend qu'une minute. Vous pouvez aussi devenir membre du Club des amis d'Iwacu, ce qui vous ouvre un accès illimité à toutes nos archives ainsi qu'à notre magazine dès sa parution au Burundi.

Editorial de la semaine

Pour plus de transparence dans nos exportations

Le manque à gagner est énorme : « Plus de quarante millions dollars sont détournés chaque année dans la vente du café ». Ce constat glaçant d’un montant colossal malignement subtilisé est celui du Chef de l’Etat, Evariste Ndayishimiye, lors de la (…)

Online Users

Total 3 053 users online