http://www.iwacu-burundi.org/wp-content/uploads/2018/01/USmerged.pdf

Uongozi wa Jumuia ya kiislamu nchini Burundi (COMIBU) wabadilishwa

20-09-2011

Baraza kuu la mashehe nchini Burundi lilizinduwa hio jana ijuma tatu tarehe 19 septemba 2011 shughli za kamati mpya ya uongozi wa Jumuia ya kiislamau nchini Burundi, hayo ni kufuatia mkutano wa dharura uliofanyika hapo septemba 11.

Maamuzi ya kikao hicho yalikua ni kusimamisha kikazi kiongozi wa muda wa Baraza kuu hilo la mashehe, Sheikh Shabani Omar na kiongozi wa Jumuia ya kiisilamu nchini Burundi, Sadiki Kajandi. Kwa mujibu wa kiongozi mpya wa COMIBU, Alhaj Haruna Nkunduwiga, mabadiloko hayo yalitokana na uelewano mdogo baina viongozi wa zamani wa COMIBU, ubadhirifu na hasa ukiukwaji wa taratibu za kamati ya uongozi wa Jumuia ya kiisilamu nchini Burundi.

Licha ya hayo kiongozi wa zamani wa Jumuia ya kiisilamu nchini Burundi, Sadiki Kajandi aliyeng’atuliwa madarakani alionekana kuyapinga maamuzi hayo. Na jambo hilo linaungwa mkono na waziri wa Burundi wa mambo ya ndani, Edourad Nduwinama. Upande wake anasema kikao hicho cha Baraza kuu la mashehe kilifanyika kinyume na sheria. Kiongozi mpya wa COMIBU, Alhaj Haruna Nkunduwiga anakumbusha kua ni jukumu la waislamu wenyewe kuyatanzuwa matatizo yanayojitokeza katika jamii yao.

Aliwatolea wito viongozi wa zamani wa Jumuia ya kiislamau nchinu Burundi (COMIBU) akiwataka watekeleze wajibu wao kwa kukubali uamzi wa Baraza kuu la mashehe huku akiwaomba kuwatambuwa viongozi wapya ikiwa ni pamoja na Sheikh Ismaïl Nayiburundi Dunia, kiongozi mpya wa Baraza kuu la mashehe na Alhaj Haruna Nkunduwiga, kiongozi mpya wa COMIBU.

Publicité