Dimanche 05 mai 2024

Archives

Cankuzo au Guantanamo ?

05/05/2013 Commentaires fermés sur Cankuzo au Guantanamo ?

Raia wanaoshakiwa kuendesha ’’vitendo vya kigaidi’’ wazidi kukamatwa na wote kwa ujumla wanapelekwa huko Cankuzo, mashariki mwa Burundi kulikozuka ’’kundi lipya la wapiganaji’’. Kanali Pierre Claver Kabirigi anadai kua kiongozi wa kundi hilo la waasi.

<doc2281|left>Kwa mujibi wa Pierre Claver Mbonimpa, kiongozi wa shirika liitwalo APRODH linalotetea haki za binadamu na za wafungwa, ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Burundi, raia wanaoshakiwa kuyumbisha usalama kulaumiwa kua wanashiriki katika vitendo vya kigaidi. Na watu hao, baadhi yao baada tu ya kukamatwa wana pelekwa huko Cankuzo, na haijulikane ikiwa mkoa huo umekwisha kuwa eneo la ugaidi, anasema mwanaharakati huyo wa haki za binadamu.

Msako ulioanzishwa na polisi kwa ushirikiano na idara ya upelelezi tangu wiki iliyopita umeisha pelekea watu wasiopungua 40 pakiwemo mwandishi wa redio Bonesha FM, Hassan Ruvakuki kutiwa ndani. Msako huo ni hasa katika mikoa ya Muyinga, Ngozi, Karuzi n Cankuzo. Baadhi ya watu hao ni waalimu, na ni wafuasi wa chama cha FNL watiifu wa Agathon Rwasa.

Kando ya shutma kua watu hao walishiriki katika ’’vitendo vya kigaidi’’, wengine wanashakiwa kua wanashirikiana na ’’kundi lipya la waasi’’ lililozuka huko mkoani Cankuzo mashariki mwa Burundi. Kanali Pierre Claver Kabirigi anadai kuwa kiongozi wa kundi hilo liitwalo FRD-Abanyagihugu.

Mkoa ‘’’unaotia fora’’ ni Muyinga ambapo kulikamatwa watu 18 pakiwemo mwanamke mmoja ambae aliwahi kuwa mbunge wa chama cha Sahwanya-FRODEBU. Katika msako ulioendeshwa kwenye nyumba ya mbunge huyo wa zamani kulikamatwa nyaraka mbalimbali na picha ikimuonesha mama huyo akiwa pamoja na mbunge Kanali Pierre Claver Kabirigi anaedai kuwa kiongozi wa kundi hilo lippya la waasi liitwalo FRD-Abanyagihugu, huku mwandishi wa redio Bonesha FM Hssan Ruvakuki akiwa na maikriphoni akiwahoji. Katika nyaraka hizo kulikamatwa pia orodha ya watu hao wanaoshakiwa kuwa na ushirikiano fulani na Kanali Pierre Claver Kabirigi.

Huko mkoani Ngozi kulikamatwa hio jana walimu 2, wote hao ni wafuasi wa chama cha FNL watiifu wa Agathon Rwasa. Mmoja ni kutoka tarafa ya Ruhororo, ni naibu kiongozi wa shu na ni mwanamemba wa halmashahuru ya tarafa hio. Mwengine ni kutoka tarafa ya Mwumba. Mwalimu huyo alikamatwa bila waranti.

Na huko mkoani Karuzi kumeishatiwa nguvuni watu 7, baadhi yao ni waalimu. Wote kwa jumla ni wafuasi wa chama cha FNL watiifu wa Agathon Rwasa. Miongoni mwao kuna mwanamke mmoja ambae amekamatwa huku akiwa na mtoto mchanga. Wote hao walikamatwa pasina waranti.

Na huko mkoani Cankuzo mashariki mwa Burundi kumeisha kamatwa watu 9 tangu tarehe 21 mwezi novemba. 8 miongoni mwao ni wafuasi chama cha FNL watiifu wa Agathon Rwasa na mmoja ni kutoka chama cha UPD-Zigamibanga cha upinzani.

A nos chers lecteurs

Nous sommes heureux que vous soyez si nombreux à nous suivre sur le web. Nous avons fait le choix de mettre en accès gratuit une grande partie de nos contenus, mais une information rigoureuse, vérifiée et de qualité n'est pas gratuite. Nous avons besoin de votre soutien pour continuer à vous proposer un journalisme ouvert, pluraliste et indépendant.

Chaque contribution, grande ou petite, permet de nous assurer notre avenir à long terme.

Soutenez Iwacu à partir de seulement 1 euro ou 1 dollar, cela ne prend qu'une minute. Vous pouvez aussi devenir membre du Club des amis d'Iwacu, ce qui vous ouvre un accès illimité à toutes nos archives ainsi qu'à notre magazine dès sa parution au Burundi.

Editorial de la semaine

La soif d’aujourd’hui

Au Burundi, pays de tradition brassicole, la bière est reine. Pour la majorité de Burundais, un évènement excluant l’alcool n’en est pas un. Dans la joie comme dans le malheur, en famille ou entre amis, la bière est obligatoire. Elle (…)

Online Users

Total 4 711 users online