http://www.iwacu-burundi.org/wp-content/uploads/2018/02/US-13FEV.pdf

Ban Ki-moon anaomba kutumwe nchini Somalia askari wa ziada wapatao 2500

05-06-2013

{{Hayo ni katika maagizo yaliyotolewa kwenye mkutano kuhusu mzozo wa Somalia uliofanyika bada ya Kikao cha 66 cha Umoja wa Mataifa huko New York.}} <doc1430|left>Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka Burundi, Somalia, Uhispania, Sudan, Sweden, Uturuki, China, Danemark, Djibouti, Ethiopia, Ufaransa, Ujeremani, Italy, Japan, Kenya, Norway, Urusi, Saud Arabia, Uganda, Umoja wa Afrika, Uingereza, Umarekani, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Umoja wa nchi za kiarabu na Tume ya ushirikiano wa kiislam. Waziri mkuu wa serekali ya mpito nchini Somalia, Abdiweli Mohamed Ali na kiongozi wa Tume ya Umaja wa Afrika Jean Ping walishiriki mkutano. Wajumbe hao walisisitiza umuhimu wa kuipa nguvu zaidi AMISOM, Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia kwa kuongeza idadi ya vikosi vya kurejesha amani nchini humo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alitolea wito jumuia ya kimataifa akiomba idadi ya majeshi yaliyotumwa nchini Somalia iongezwe hadi kufikia askari 12.000. Alibaini kua kunatakiwa askari wapatao 2.500 wa ziada ili idadi hio ikamilike. Aliwaomba wafadhili kusaidia Umoja wa Afrika na nchi zilizituma majeshi huko Somalia kurejesha amani. Wafadhili hao aliwataka pia washirikiane kwa dhati na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika ili uwezo kipesa na vifaa vipatikane haraka iwezekanavyo. Msemaji wa jeshi la Burundi, Colonel Gaspard Baratuza amebaini kua majeshi kutoka Burundi yako tayari kwa kuchangia katika mpango huo wa kuboresha amani nchini Somalia. Amesema hatua hio ya kuongeza idadi ya askari huko Somalia itatia nchangamoto juhudi hizo zinazofanyika za kurejesha amani. Amekiri kua askari hao wa ziada watapelekwa kwenye ngome za zamani za mapiganaji wa kundi la Al Shabaab. Msemaji huyo wa jeshi la Burundi, anaomba Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kufanya kila liwzezkanalo ili majeshi kutoka Burundi na Uganda yaliyotumwa nchini Somalia kusaka amani yarahisishiwe upande wa vifaa na mishahara.

Publicité
error: Ce contenu est protégé par le droit d\'auteur